Katibu Mkuu wa OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu amesema, ‘Kufuatia hujuma za kigaidi nchini Norway, tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia za wahanga, serikali na wananchi wa nchi hii”.
Katibu Mkuu wa OIC emetoa wito wa kuendelezwa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na ugaidi.
Wakati huo huo mshukiwa wa hujuma za kigaidi Norway amekiri kutekeleza hujuma ya ufyatuliaji risasi katika kisiwa cha Utoeya ambapo watu 87 waliuawa siku ya Ijumaa. Polisi ya Norway imesema Anders Behring Breivik pia ni mshukiwa wa hujuma ya bomu katika mji mku Oslo siku hiyo hiyo ambapo watu saba waliuawa. Mshukiwa huyo amesema yuko tayari kujieleza mahakamani.
Hujuma hizo mbili zimepelekea watu 94 kuuawa na polisi wanasema huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Breivik ni Mkristo mwenye misimamo mikali ambaye ni mfuasi wa siasa zenye kufurutu mipaka za mrengo ya kulia. Aidha katika kurasa zake za intaneti alibainisha chuki dhidi wa Waislamu, vyama vya mirengo ya kushoto na kitengo cha vijana cha chama tawala cha Leba nchini Norway.
830296