Kwa mujibu wa gazeti la Al Bayan, shughuli hizo zitajumuisha mihadhara ya kidini itakayohutubiwa na wanazuoni wa ngazi za juu wa ulimwengu wa Kiislamu. Mihadhara hiyo itaendelea hadi tarehe 20 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Imearifiwa kuwa hotuba zitatolewa kwa lugha kadhaa kwa ajili ya Waislamu wa mataifa mbalimbali wanaoishi Imarati. Mashindano ya 15 ya Kimataifa ya Qur'ani Dubai yataanza tarehe 10 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwakutanisha washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani. 834318