Kongamano hilo linasimamiwa na Jumuiya ya Qur'ani ya Saihat ikishirikiana na maulamaa na watafiti wa masuala ya Qur'ani katika Msikiti wa Rasurul Aadham SAW katika mji wa Saihat.
Kongamano hilo linalofanyika kila mwaka katika nusu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani huhudhuriwa na shakhsia mashuhuri wa mikoa ya mashariki mwa Saudia yenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia. Mada kuu ya kongamano la mwaka huu ni amani ya kijamii na ushirikiano na kuishi kwa amani jamii zenye tamaduni tofauti katika mtazamo wa Qur'ani Tukufu. 838035