Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumani Iman Meizak ametoa taarifa akisema kuwa wachezaji wa mpira wa timu za soka wanaweza kufungua katika siku ambazo wanacheza mechi na kufunga katika siku zilizosalia.
Fatuwa hiyo ambayo imeifurahisha mno Federesheni ya Mpira wa Miguu ya Ujerumani imetambuliwa na raia Waislamu na baadhi ya wachezaji wa soka wa Ujerumani kwenyewe kuwa inapingana na mafundisho ya Kiislamu. Pande hizo zimetaka fatuwa hiyo ifutwe.
Mwaka jana pia Federesheni ya Mpira wa Miguu ya Ujerumani iliwataka maulamaa wa al Azhar huko Misri kutoa fatuwa inayowaruhusu wachezaji Waislamu kufungua katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 842293