IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kuanza kesho Algeria

15:25 - August 20, 2011
Habari ID: 2174048
Mashindano ya 8 ya Kimataifa ya Hifdhi na Kiraa ya Qur'ani Tukufu yataanza kesho nchini Algeria katika mji wa Telmsan yakiwashirikisha wawakilishi wa nchi 47.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Algeria imesema kuwa Mashindano ya 8 ya Kimataifa ya Hifdhi na Kiraa ya Qur'ani yataanza kesho yakiwashirikisha wawakilishi wa nchi 47. Taarifa hiyo imeongeza kuwa nchi zote zina haki ya kuwakilishwa na karii mmoja tu na kwamba umri wa washiriki unapaswa kuwa chini ya miaka 25. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa sharti hilo la umri linawapa vijana fursa ya kudhihirisha vipawa na uwezo wao.
Wizara ya Wakfu ya Algeria imetangaza kuwa sambamba na mashindano hayo ya kimataifa, kutafanyika pia mashindano ya kitaifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani yatakayowashirikisha vijana wenye umri wa chini ya miaka 15. Mashindano haya yanafanyika kwa shabaha ya kuwahamasisha vijana kusoma na kujifunza kitabu cha Mwenyezi Mungu SW.
Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Kimataifa ya Hidhi na Kiraa ya Qur'an Tukufu ya Algeria atatunukiwa zawadi ya dola elfu kumi, mshindi wa pili atapata dola elfu 8 na mshindi wa tatu atapewa dola elfu 5.
Washiriki wote wa mashindano hayo ya kimataifa pia watatembelea maeneo na athari za Kiislamu na kihistoria za mji wa Telmsan huko magharibi mwa Ageria, kwa mnasaba wa shughuli za kutangazwa rasmi mji huo kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2011. 846538
captcha