Kwa mujibu wa tovuti ya Al Alam, Harakati ya Hizbullah imeandaa hafla ya kila mwaka ya Siku ya Quds katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh Heidar Daqmaq mkuu wa Idara ya Habari ya Hizbullah Kusini mwa Lebanon amesema hafla hiyo itafanyika katika Bustani ya Iran eneo la Marun Ar Ra'as, karibu na mpaka wa eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel. Amesema kaulimbiu ya hafla ya mwaka hii ni 'Utiifu kwa Damu, Subira na Majeruhi'.
Amesema Sayyid Hassan Nasrallah atahutubia hafla hiyo kwa njia ya video.
Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ambayo Waislamu kote duniani huonyesha mfungamano wao na Waislamu wanaodhulumiwa wa Palestina.
Imam Khomeini RA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mnamo mwaka 1979 alitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds.
847154