IQNA

Kongamano la Qur'ani lamalizika Saihat, Saudia

15:43 - August 21, 2011
Habari ID: 2174733
Jumuiya ya Qur'ani kwenye mkoa wenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia wa Saihat huko mashariki mwa Saudi Arabia imesema kuwa kongamano la 9 la kila mwaka ka Qur'ani Tukufu ambalo lilianza tarehe 15 Ramadhani limekamilisha shughuli zake.
Sherehe za kuhitimisha kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na maulamaa na watafiti wa masuala ya Qur'ani wa Saudi Arabia katika Msikiti wa Rasulul Aadham, zimehutubiwa na mkurugenzi wa kongamano hilo Abdul Jalil al Rashid.
Ustadh Abdul Jalil al Rashid ameashiria maelewano na hali ya kuishi kwa amani inayoshuhudiwa sasa kati ya Waislamu na kusema kuwa hali hiyo inasaidia katika shughuli za ustawi na ujenzi, jambo ambalo ni lengo la wanadamu wote.
Amesema kuwa ni jambo la kawaida kuwepo hitilafu za kimitazamo kati ya Waislamu, jambo suala ambalo pia limeashiriwa katika Qur'ani na Suna za Mtume SW.
Amesisitiza kuwa serikali zinazotawala nchi mbalimbali duniani zinajiona kuwa pweke na mbali na wananchi na matakwa yao na kwa msingi huo zinatumia silaha ya kuzusha hitilafu za kimadhehebu kati ya Waislamu wa nchi moja.
Kongamano la kila mwaka la Qur'ani Tukufu ambalo hufanyika kuanzia tarehe 15 Ramadhani katika mkoa wenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia hujadili masuala muhimu kama suluhu ya kijamii na maisha ya amani na udugu kati ya jamii zenye tamaduni tofauti katika mtazamo wa Qur'ani Tukufu. 847254
captcha