IQNA

21:21 - August 23, 2011
Habari ID: 2175469

Hizbullah yataka kutafutwa sehemu alikofungwa Musa Sadr

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imetoa taarifa ikiwapongeza wanamapinduzi wa Libya kutokana na ushindi walioupata dhidi ya dikteta Muammar Gaddafi na kuwataka wafanye juhudi za kusaidia kutafuta na kuweka wazi sehemu anakozuiliwa Imam Musa Sadr.

Taarifa hiyo imewaomba viongozi wa mapinduzi hayo kufanya kila wanaloweza ili kutafuta sehemu hiyo kwa ajili ya kuachiliwa huru shakhsia huyo muhimu wa Lebanon pamoja na wasaidizi wake wawili, Sheikh Ya'qub na Badr ad-Deen, ambao walitekwa nyara na dikteta Muammar Gaddafi.
Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon pia amemtumia barua Mustafa Abdul Jalil, Mkuu wa Baraza la Wanamapinduzi wa Libya akiwapongeza kwa ushindi wao dhidi ya dikteta huyo wa Libya. Amesema katika barua hiyo kwamba wanamapinduzi wa Libya wamepata ushindi katika hali ambayo wananchi wa Lebanon tokea mwaka 1978 wamekuwa wakiishi na majonzi ya kutekwa nyara Imam Musa Sadr na kwamba ufunguo wa kutafutwa kiongozi huyo wa zamani wa mapambano ya Lebanon uko mikononi mwa wanamapinduzi hao.
Chama cha Amal cha Lebanon pia kimetoa taarifa kikiitaka serikali ya Lebanon kutuma ujumbe wa ngazi za juu nchini Libya ili kujadiliana na viongozi wapya wa nchi hiyo kuhusu kadhia hiyo. 848149
captcha