IQNA

Wamisri wataka balozi wa Israel afukuzwe nchini humo

20:08 - August 27, 2011
Habari ID: 2177660
Viongozi na wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi ya wananchi wa Misri walikusanyika jana ndani ya msikiti wa al Azhar wakitaka kufukuzwa balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini humo.
Habari zinasema kuwa mkusanyiko huo ulifanyika ndani ya Msikiti wa al Azhar kuonyesha upinzani dhidi ya uhalifu na jinai za Israel na ulitoa wito wa kufukuzwa balozi wa utawala huo ghasibu nchini Misri.
Waandamanaji hao waliitaka serikali ya Cairo isimamishe uuzaji wa gesi ya Misri kwa utawala ghasibu wa Israel na kulaani jinai za utawala huo katika mpaka wa Misri na Ukanda wa Gaza.
Mwenyekiti wa chama cha Amal Majdi Hussein mesisitiza mbele ya mjumuiko huo kwamba eneo la Sinai linapaswa kuondolewa katika udibiti wa Israel. Ameongeza kuwa baada ya ushindi wa mapinduzi ya wananchi, Misri inapaswa kuchukua hatua kali zaidi za kukabiliana na uhalifu na uchokozi wa Israel.
Kiongozi wa chama cha Amal amesisitiza kuwa kunyamaza kimya kwa serikali ya Misri mbele ya jinai na mauaji yaliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika mpaka wa nchi hiyo na Ukanda wa Gaza ni jambo ambalo haliwezi kukubaliwa. 850492

captcha