Akizungumza katika mahojiano kuhusu urithi na hadhi ya Kiongozi huyo shahidi, Alexander Dugin, mwanafalsafa na mwanadharia mashuhuri wa Urusi, alionyesha masikitiko makubwa kwa taifa la Iran kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi huyo, tovuti ya Umoja wa Redio na Televisheni ya Kiislamu imeripoti.
“Kama Mkristo wa Kiorthodoksi ambaye nimekuwa nikisoma kuhusu Ushia na hasa Uislamu ulivyo Iran kwa miaka mingi, naona kuuawa shahidi si mateso bali ni kushuhudia ukweli. Katika mapokeo yetu, kanisa limejengwa juu ya miili ya mashahidi, na kuuawa shahidi ni muujiza ambao Mungu huutunuku kuwepo kwa mwanadamu. Mashahidi, akiwemo Ayatullah Khamenei, si waathiriwa tu, bali ni mashahidi wa kweli ambao, kwa sadaka yao, wanaharakisha kuja kwa Imam Mahdi (AS), mwokozi aliyeahidiwa. Kifo hiki si cha bure; bali kinaunda msingi wa kuwepo kwa wakati ujao, na utamaduni wa Iran unaelewa ukweli huu kuliko mtu yeyote,” alisema.
Akirejelea muundo wa Wilayat-e-Faqih, au mfumo wa Faqihi Mtawala ambao ndio msingi wa utawala wa Mapinduzi ya Kiislamu, Dugin alisisitiza kuwa sifa muhimu zaidi ya mfumo wa kisiasa wa Iran ni kuwepo kwa kiongozi wa kiroho katika uongozi ambaye anawajibika mbele ya Mungu.
“Ayatullah Khamenei hakuwa mwanasiasa na mtaalamu mashuhuri pekee, bali pia alikuwa ishara ya kanuni ya kiroho. Kuwepo kwake kulikuwa kilele kilichotoa maana kwa mfumo wa asili wa kisiasa. Kupaa kwa shahidi huyu kulifungua mlango wa kutokufa; mlango ambao sasa unaelekeza kwenye ulimwengu wa nuru .
Tukio hili litaleta mabadiliko makubwa na Iran ya kishujaa itasimama na kushinda dhidi ya Magharibi yote.”
Akijibu swali kuhusu uvamizi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, mwanafalsafa huyo wa Urusi alisema kuwa hakuna maana yoyote ya kisiasa au kijeshi katika kuua watoto na raia wa Iran na ni wazi kuwa Magharibi ya kisasa ni ustaarabu wa Baali na Mpinga Kristo (Antichrist), ambao hauna lengo lingine isipokuwa kuua wasio na hatia.
“Kwa kufanya sherehe ya kuchoma sanamu lililoshabihiana na Baali, Iran ilifichua hali halisi ya utawala wa Marekani na Wazayuni. Leo, nchi mbili za Iran na Urusi, kama mstari wa mbele wa mapambano, zinapigana ustaarabu huu mwovu. Vita hivi ni vita dhidi ya adui wa ubinadamu, na ushindi ni wa wale walio upande wa Mungu. Mateso ya Mashia na mashahidi wa Urusi yatalipwa hivi karibuni na matunda yake yatafichuka.”
Akijibu swali kuhusu msimamo imara wa Wairani, Dugin alisema: “Kile ambacho ulimwengu unashuhudia leo ni umoja usio na kifani wa taifa la Iran; wote, kutoka asili zote za kitamaduni na kiakili, wameungana chini ya kaulimbiu ‘Nitakufa kwa ajili ya Iran’.”
“Utayari huu wa kujitolea unaashiria ushindi wa kiroho usioweza kubadilishwa wa Iran. Kinyume chake, tabia ya baadhi ya nchi nyingine za Kiislamu zinazoshirikiana na Israel ni ya aibu. Nawaambia Waislamu wa dunia: Jiungeni na jihadi ya kweli dhidi ya Mpinga Kristo na muiunge mkono Iran, ambayo imepandisha bendera nyeusi ya Khorasan. Naamini kwamba kudhihiri kwa Mahdi (amani iwe juu yake) kumekaribia.”
Akiwahutubia taifa la Iran, Dugin alisema, “Sisi, watu wa Urusi, tunawaheshimu kwa mioyo yetu yote. Msiwe na matumaini Magharibi, kwa sababu mkataba na shetani umesainiwa kwa damu. Simameni pamoja na mwe imara, kwa sababu ushindi ni wetu, na mashahidi wetu ni mashahidi wa milele wa ukweli huu.”
3498067