IQNA

Wageni kutoka mataifa mbalimbali kufika Iran kwa ajili ya mazishi ya Kiongozi Shahidi

16:37 - June 30, 2026
Habari ID: 3482423
baraza
IQNA – Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, ametangaza kuwa ujio wa maafisa na wajumbe wa kigeni wanaotarajiwa kushiriki katika hafla ya k mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, utaanza rasmi siku ya Ijumaa.

Akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri siku ya Jumapili, Aref amesisitiza kuwa mipango madhubuti imekamilika kwa ajili ya kuwakaribisha wageni hao na kuratibu ushiriki wao katika hafla hiyo ya kihistoria.

Aref alimuenzi Kiongozi huyo shahidi kwa heshima kubwa, akibainisha kuwa shughuli hiyo ya kuwaaga na mazishi yake huenda ikawa tukio muhimu zaidi katika karne ya 21.

“Wananchi ndio wenyeji wakuu wa hafla hii na wako mstari wa mbele,” amesema Aref, akiongeza kuwa taasisi za serikali, mashirika ya umma, na asasi zisizo za kiserikali zote zimejitolea kwa dhati ili kuhakikisha tukio hili linafanikiwa kwa ukamilifu.

Akielezea utayari wa nchi kwa ajili ya hafla hiyo, Aref ameongeza kuwa tahadhari maalum na maandalizi ya usalama yamezingatiwa ili kuhakikisha kuwa msongamano wa watu hauletei madhara yoyote. “Insha’Allah, shughuli hii itafanyika katika mazingira ya utukufu na amani, huku tukizingatia masuala ya usalama na ustawi wa wananchi,” alisema.

Ibada ya mazishi ya Kiongozi huyo Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu itafanyika mjini Tehran siku ya Jumamosi na Jumapili, tarehe 4-5 Julai 2026.

Ikumbukwe kuwa, Ayatullah Khamenei aliuawa shahidi kufuatia vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran mnamo Februari 28. Uchokozi huo, ambao pia ulipelekea kuuawa maafisa wa ngazi ya juu na raia wengi wasio na hatia, ulipelekea Iran kujibu mapigo kwa kufanya mashambulizi yasiyopungua 100 ya kulipiza kisasi dhidi ya maeneo nyeti na ya kimkakati ya Marekani na Israel. Hatua hiyo ya kulipiza kisasi ilipelekea Marekani kutangaza usitishaji wa mapigano wa upande mmoja mnamo Aprili 7.

3498016

captcha