IQNA

Maelfu wahudhuria maombolezo ya Muharram Tehran, wamkumbuka Kiongozi aliyeuawa Shahidi

19:28 - June 22, 2026
Habari ID: 3482391
IQNA – Maombolezo ya Muharram kwa ajili ya Imam Hussein (AS) yamefanyika karibu na Husseiniyeh ya Imam Khomeini (RA) jijini Tehran, siku ya Jumapili jioni.

Maelfu ya waumini kutoka tabaka mbalimbali za jamii walihudhuria ibada hiyo ya maombolezo karibu na mahali ambapo aliuawa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu  Ayatullah Sayyid Ali Khamenei 10 Ramadhani sawa na 28 Februari.

Mwaka huu, hafla hiyo imefanyika kwa usimamizi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei.

Katika hafla hiyo ya Jumapili usiku, Hujjatul Islam Seyed Mir Hashem Hosseini alitoa hotuba yenye mada ya “Mahesabu ya Maisha na Umaanawi Katika Maisha.”

Katika hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia dhana za kiroho na kumtanguliza Mwenyezi Mungu pamoja na ahadi Zake tukufu sambamba na mahesabu ya kimaada katika maisha ya mtu binafsi na kijamii. Alibainisha kuwa ulinzi mtakatifu wa taifa la Iran katika ‘Vita vya Ramadhan’ unatokana na mafunzo ya tukio kubwa la Karbala pamoja na kujitolea Imam Hussein (AS) na wafuasi wake waaminifu.

Aliongeza kuwa 'Vita vya Ramadhan' ni mfano dhahiri wa kuzingatia umaanawi sambamba na mahesabu na maandalizi ya kimaada.

Aidha, Mehdi Rasouli aliimba kasida za maombolezo (latmiya) kuomboleza msiba wa Imam Hussein (AS), mashahidi wa Karbala, na Shahidi Imam Khamenei, huku akiwaenzi na kuwataja kwa heshima mashahidi wa ngazi za juu wa Vita vya Ramadhan.

3497928

Habari zinazohusiana
captcha