IQNA

Rais Pezeshkian: Mahudhurio Makubwa katika Mazishi ya Kiongozi Shahidi ni ‘Jibu Imara’ kwa ubeberu na ugaidi

17:27 - July 02, 2026
Habari ID: 3482429
IQNA-Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa umati mkubwa wa wananchi utakaojitokeza katika shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, utakuwa ni “jibu madhubuti” dhidi ya vitendo vya kigaidi, ukatili, na mbinu za kibeberu. Aidha, amebainisha kuwa tukio hilo litakuwa ni dhihirisho la wazi la umoja wa taifa la Iran na dhamira yake isiyotetereka katika kulinda uhuru na heshima ya nchi.

Rais Pezeshkian ameyasema hayo katika ujumbe wake wa  leo Alhamisi kwa taifa la Iran, wakati wa maandalizi ya hafla za kumwaga na kumzika Imam Khamenei, ambaye aliuawa shahidi mnamo Februari 28, siku ya kwanza ya vita vya kichokozi Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Rais ameonyesha imani yake kuu juu ya nafasi ya wananchi katika kipindi hiki cha mabadiliko, akibainisha kuwa katika hafla hii adhimu ya mazishi, taifa la Iran litathibitisha tena utiifu wake kwa njia na malengo makuu ya Kiongozi huyo aliyeawa shahidi.

Rais amesisitiza kuwa ushiriki wa wananchi katika tukio hili la kihistoria utathibitisha, bila shaka yoyote, uaminifu wao kwa njia iliyowekwa na marehemu Kiongozi.

Ameongeza kuwa kifo cha kishahidi cha Ayatullah Khamenei kimeacha simanzi nzito si tu miongoni mwa Wairani, bali pia katika ulimwengu wa Kiislamu na mataifa yote yanayopigania uhuru. Hata hivyo, amesisitiza kuwa pigo hilo limefunua ukweli usiopingika kwamba misingi imara ya mfumo wa Kiislamu imejengeka juu ya “nguzo madhubuti za imani, malengo matukufu, na utashi wa taifa kubwa.”

Rais Pezeshkian ameusifu upeo wa mawazo na utendaji wa Shahidi Imam Khamenei katika kulinda uhuru wa Iran, huku akikuza demokrasia ya kidini na utamaduni wa muqawama (mapambano) katika baadhi ya vipindi vyenye changamoto kubwa zaidi katika historia ya kisasa ya taifa la Iran.

Amesema kuwa jina, mawazo, na mafanikio ya Shahidi Ayatullah Khamenei bila shaka yatasalia milele katika kumbukumbu ya kihistoria ya taifa la Iran na dhamiri ya watu wote wanaopigania haki duniani kote.

Rais ametoa wito kwa Wairani wote, bila kujali kabila, dini, au mwelekeo wa kisiasa, kujitokeza kwa wingi katika shughuli za mazishi ili kuonesha taswira ya umoja wa kitaifa na uaminifu kwa malengo matukufu ya mfumo wa Kiislamu.

4361700

Habari zinazohusiana
captcha