Akizungumza katika mahojiano na IQNA, Jalil Bayt Mashali alisema: “Tutatumia vyema fursa hii kuitambulisha tabia ya Kiqur’ani ya Kiongozi Shahidi kwa namna inayostahiki, na jambo hili litatekelezwa kupitia warsha na mikutano ya kitaalamu.”
Mahojiano hayo ni kama ifuatavyo:
IQNA: Kwanza, tafadhali elezea hatua za maandalizi na utekelezaji wa mashindano hadi sasa?
Moja ya juhudi nzuri za taasisi ya kisayansi na ya kimapinduzi ya Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) katika uwanja wa Qur’ani Tukufu ni kuandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi Waislamu. Shughuli za utekelezaji wa toleo la saba zimekuwa zikiendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja. Matukio ya hivi karibuni, yakiwemo Vita vya Siku Kumi na Mbili na Vita vya Ramadhani, vilisababisha mchakato huu kukatizwa mara kwa mara, lakini tulijitahidi kuendelea kulingana na ratiba iliyokuwa imepangwa.
Hatua ya awali ya toleo hili ilianza kwa ushiriki wa wawakilishi kutoka nchi 76, na kwa sasa baada ya kukamilika kwa hatua ya nusu fainali, watu 25 wamefika hatua ya mwisho katika kipengele cha usomaji wa Qur’ani. Katika sehemu ya teknolojia jumla za Qur’ani, kati ya kazi 45 zilizowasilishwa kwa sekretarieti, kazi 10 zimechaguliwa kufika hatua ya mwisho baada ya tathmini ya majaji. Pia, wahifadhi 26 wa Qur’ani nzima walishindana katika hatua ya nusu fainali, na majina ya wale waliyoingia fainali yatatangazwa hivi karibuni.
IQNA: Je, mnatarajia kuandaa hatua ya mwisho ya mashindano haya kwa njia ya ana kwa ana?
Iwapo hali itakuwa nzuri, tutafanya hatua ya mwisho kwa njia ya ana kwa ana. Vinginevyo, kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Qur’ani na hasa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), tutabuni mbinu mpya kwa kutumia mazingira ya mtandaoni, ambapo hatua hiyo itafanyika katika mfumo wa programu ya mkusanyiko kwa muda wa takribani wiki moja.
IQNA: Katika toleo la saba tunaona kuongezwa kwa sehemu mpya. Tafadhali elezea zaidi kuhusu sehemu hii.
Katika matoleo sita yaliyopita, mashindano yalikuwa katika nyanja mbili: usomaji wa Qur’ani na hifzi ya Qur’ani nzima. Katika toleo hili, kwa kuzingatia hadhira maalumu ya tukio hili, ambao ni wanafunzi, na pia upana wa shughuli zao katika mifumo mipya ya kiteknolojia, tuliongeza kipengele cha “Teknolojia na Uzalishaji wa Jumla wa Qur’ani”. Kipengele hiki kiko karibu zaidi na mazingira ya fikra na ubunifu wa wanafunzi. Kati ya kazi 45 zilizowasilishwa katika sehemu hii, kazi 10 bora zimechaguliwa kuingia hatua ya mwisho kwa ajili ya tathmini.
IQNA: Kutokana na maoni ya jumla ya majaji, imeonekana kuwa washiriki wengi hawafahamu vizuri kanuni za mashindano haya. Je, kuna hatua zilizochukuliwa kuhusu hili?
Kabla ya kuanza kwa mashindano, kanuni zilishirikishwa katika lugha tatu, Kiingereza, Kiajemi na Kiarabu, kupitia njia na majukwaa ya habari ya mashindano katika mtandao kwa ajili ya kuwafahamisha washiriki na wadau wengine wa utekelezaji. Hata hivyo, ikiwa hatua ya mwisho itafanyika ana kwa ana, tutafanya vikao vya maelekezo na warsha kuhusu suala hili. Na iwapo mashindano yatafanyika kwa njia ya mtandaoni, tutatayarisha na kusambaza maudhui ya ufafanuzi kabla ya kuanza kwa hatua ya mwisho ili kuwafahamisha washiriki zaidi.
IQNA: Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi Waislamu yameleta fursa maalumu ya kufafanua na kutambulisha shakhsia ya Kiqur’ani ya Kiongozi Shahidi, ambaye pia alikuwa miongoni mwa waungaji mkono wakubwa wa wanaharakati na watu wa Qur’ani. Mtawezaje kuitumia vyema fursa hii?
Kwa masikitiko makubwa tulimpoteza Kiongozi Mkuu wa Umma wa Kiislamu, aliyekuwa miongoni mwa wabeba bendera wakuu wa kutetea Qur’ani Tukufu, wakati wa Vita vya Tatu vya Kulazimishwa. Kwa hiyo, ni muhimu kutumia kila fursa iliyopo kuelezea shakhsia hii tukufu, hasa upande wa tabia yake ya Kiqur’ani. Mashindano haya yanatoa nafasi nzuri kwa jambo hili, na kwa hiyo tunakusudia
4358919