IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya akinamama na watoto Qatar

20:50 - August 27, 2011
Habari ID: 2177661
Mashindano ya 11 ya kimataifa ya Qurani Tukufu makhsusi wa ajili ya akinamama na watoto yamefanyika katika kituo cha QIIC nchini Qatar.
Mashindano hayo ambayo yamefanyika kwa wakati mmoja pia katika madrasa ya Hamza bin Abdul Muttalib mjini Doha na kituo cha Hannan katika mji wa Dahan yameshirikisha na maelfu ya watu.
Mashindano hayo ya Qur'ani yamefanyika katika sehemu tatu za hifdhi ya sura ya Maidah, hifdhi ya suratu Luqman na hifdhi ya suratul Mutaffifin kwa lengo la kuwahamasisha watu kusoma Qur'ani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Washindi wa mashindano hayo watatangazwa katika sherehe itayofanyika katika sikukuu ya Idul Fitr.
Kituo cha QIIC cha Qatar kilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha usomaji Qur'ani Tukufu na kina madrasa 24 kote nchini humo. 850403


captcha