Mashindano ya Qur'ani kwa njia ya televisheni yaliyopewa jina la Aliif, Laam, Miim yamekuwa yakifanyika nchini Pakistan kupitilia kanali ya televisheni ya Geo Tv.
Programu hiyo ya Tv ya mashindano ya Qur'ani Tukufu ambayo inashabihiana na programu ya televisheni inaoitwa 'Nani Anataka kuwa Milionea?, inafanyika kwa anwani ya 'Nani Anataka Kwenda Hija.'
Washiriki katika programu hiyo wanajibu maswali 15 kuanzia maswali mepesi hadi magumu katika wakati maalumu ulioainishwa na iwapo mshiriki atashindwa kujibu maswali katika muda huo huondolewa katika mashindano.
Wasindi katika mashindano hayo watatunukiwa zawadi nono ikiwa ni pamoja na nyumba, gharama za kwenda kuhiji Makka na fedha taslimu euro elfu 20. 851142