Ensaiklopidia ya nchi za Kiislamu iliyoandikwa na kutayarishwa na Ashur Shurafi, mtaalamu wa masuala ya Kiislamu, imechapishwa huko Algeria.
Ensaiklopidia hiyo yenye juzuu mbili zilizo na kurasa 450 kila moja inajumuisha maudhui na mambo mbalimbali yanayohusiana na ustaarabu wa Kiislamu kwa mtazamo mpya.
Mwandishi wa ensaiklopidia hiyo amekusanya humo masuala yote ya kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi ya nchi zote 57 wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, masuala ambayo yanaandamana na picha za utamaduni na mila za mataifa husika.
Maelezo kuhusu miji mikuu ya nchi za Kiislamu na historia fupi ya maisha ya viongozi pamoja na mapinduzi yaliyotokea katika nchi hizo ni baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika kitabu hicho cha maarifa. 851507