Khalifa bin Salman Aal Khalifa, Waziri Mkuu wa Bahrain amefutwa kazi kwa lengo la kutuliza malalamiko ya wananchi wa nchi hiyo, katika hali ambayo muungano wa Mapinduzi ya Februari 14 ungali unasisitiza juu ya kuangushwa mfumo mzima wa utawala wa nchi hiyo.
Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa Bahrain amechukua uamuzi wa kumfukuza kazi waziri mkuu huyo kutokana na pendekezo lililotolewa na mfalme wa Qatar na watawala wa Imarati kwa madhumuni ya kumaliza mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Waziri mkuu huyo amefutwa kazi akiwa nje ya nchi na ukoo wa kifalme wa Bahrain haujasema lolote kuhusiana na suala hilo.
Licha ya mabadiloko hayo ya ksiasa, lakini muungano wa Februari 14 umetangaza wazi kuwa haukubaliani na pedekezo hilo la Qatar na kusisitiza juu ya kuvunjwa mfumo mzima wa utawala wa Bahrain. 851535