IQNA

Mashindano ya Qur'ani huleta Umoja wa Kiislamu

14:46 - August 29, 2011
Habari ID: 2178747
Kuandaliwa mashindano ya Qur'ani hutoa msukumo wa umoja miongoni mwa Waislamu duniani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma katika Radio Qur'an Muhammad Hussein Husseinzadeh alipohutubia awamu ya 10 ya Mashindano ya Qur'ani na Adhana katika Kisiwa cha Kish kusini mwa Iran. Amesema mashindano ya Qur'ani ni katika hatua za kufuata mafundisho ya Mtume SAW.
Amesisitiza juu ya umuhimu wa kujifunza tarteel na hifdhi ya Qur'ani Tukufu na vilevile adhana. Amekumbusha kuhusu muongozo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei kuhusu kufikia lengo la kuwa na watu milioni 10 walio hifadhi Qur'ani kikamilifu nchini Iran na kusema kuwa Radio ya Qur'an inajitahidi kutekeleza jukumu lake kuhusu suala hilo.
850618
captcha