Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Muhammadi akizungumza na IQNA amesema kuwa, wakati Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alipokutana na Jamii ya Wanaharakati wa Qur'ani nchini hivi karibuni alisisitiza kuhusu suala la kuongezwa idadi ya waliohifadhi Qur'ani nchini Iran.
Amesema Shirika la Waqfu sasa linatoa kipaumbele kwa suala la kutekeleza nasaha za Kiongozi Muadhamu. Amesema, sasa hivi kuna mikakati ya kuongeza idadi ya waliohifadhi Qur'ani nchini.
851491