IQNA

Wafungwa wahitimisha Qur'ani mara 130 elfu katika jela za Iran

15:19 - August 30, 2011
Habari ID: 2179188
Mkuu wa Darul Qur'an za Idara ya Magereza ya Iran amesema wafungwa wamehitimisha Qur'ani Tukufu mara 130 elfu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kote nchini.
Akizungumza na IQNA, Mohammad Hassan Rabani Mkuu wa Darul Quran katika Idara ya Magereza nchini Iran amesema, kwa mujibu wa mpango uliokuwepo, Qur'ani imehitimishwa mara 130 katika magereza nchini kupitia makundi ya watu 30 na 60.
Ameongeza kuwa magereza pia yalikuwa na programu ya kutoa mafunzo ya Qur'ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
851831
captcha