IQNA

Vituo vya Qur’ani katika mabustani ya Tehran

11:12 - September 03, 2011
Habari ID: 2180146
Vituo vya Qur’ani Tukufu vitafunguliwa katika mabustani yote ya mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran.
Hujjatul Islam Hamid Mohammadi , Mkuu wa Kituo cha Uratibu na Ustawi wa Shughuli za Qur’ani katika Baraza la Mji wa Tehran amemwabia mwandishi wa IQNA kuwa mpango huo utatekelezwa kutokana na juhudi za baraza hilo pamoja na baraza la mji.
Ameongeza kuwa taasisi nyinginezo ikiwa ni pamoja na vyuo vya kidini na vituo vya Qur’ani vinashirikiana katika mpango huo.
Hujjatul Islam Mohammadi amesema mpango huo unalenga kukidhi mahitaji ya jamii na kustawisha utamaduni wa Qur’ani. Amesema kuwa mpango huo tayari umeshaanza katika baadhi ya mabustani ya Tehran.
Mji wa Tehran wenye wakazi zaidi ya milioni 12 una maelfu ya mabustani ambayo yameenea katika mitaa yote.
852558
captcha