IQNA

Insiklopidia ya maana na istilahi za Qur'ani Tukufu yachapishwa na ISESCO

17:56 - September 05, 2011
Habari ID: 2181904
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO limechapisha insiklopidia ya manaa na istilahi za Qur'ani Tukufu katika juzuu mbili.
Kitabu hicho kimendikwa na Muiraq Hadi Hassan Hamoudi na kuchapishwa chini ya usimamizi wa ISESCO.
Utangulizi wa kitabu hicho ambacho juzuu yake ya kwanza ina kurasa 585 na juzuu ya pili ina kurasa 545, umeandikwa na Katibu Mkuu wa ISESCO Abdul Aziz Bin Othman Al-Tuwaijri.
Al Tuwaijri amesema katika utangulizi huo kwamba istilahi na maana za aya za Qur'ani zilipewa umuhimu mkubwa katika kipindi chote cha histora kutokana na haja ya kutaka kuelewa Qur'ani, kutekeleza mafundisho yake, kujua siri za muujiza wa kitabu hicho, kufahamu fasihi na balagha yake na kadhalika.
Ameongeza kuwa kitabu hicho hiyo inakusanya mitazamo tofauti kuhusu maana za istilahi za Qur'ani Tukufu na mwandishi wake amefanya jitihada za kutaja na kukusanya istilahi zilizotumiwa katika tafsiri mbalimbali za Qur'ani. 854466

captcha