Haya ni kwa mujibu wa Ali Pashaee, Mkuu wa Taasisi ya Familia na Qur’ani ya Iran. Pashaee ametoa wito kwa maafisa wa Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu kushirikiana na taasi za Kiislamu nchini kama vile Shirika la Ustawi wa Kiislamu ili kuhakikisha kuwa mafundisho ya Qur’ani yanaonekana kivitendo katika maisha ya kila siku ya wananchi.
Amesema pamoja na kuwepo vituo 3000 vikubwa vya Qur’ani nchini Iran bado juhudu zaidi zinahitajika ili kuimarisha mafundisho ya Qur’ani na kuhakikisha kuwa miongozo wa kitabu hicho kitukufu inatekelezwa katika maisha ya kila siku.
‘Leo maadui wanajaribu kupotosha Qur’ani Tukufu kwa mtazamo wa utekelezaji na hivyo kuna haja kwa wataalamu wa Qur’ani kuongeza juhudi katika uwanja huo. 853406