IQNA

Ran Khanzadeh:

Kuchomwa moto Qur'ani kumenihamasisha kutengeneza Qur'ani ndogo zaidi ya dhahabu

14:07 - September 08, 2011
Habari ID: 2183586
"Baada ya kushuhudia kasisi wa Kimarekani akiivunjia heshima Qur'ani kwa kuchoma moto kitabu hicho kitakatifu niliathirika mno na kuchukua uamuzi wa kutengeneza athari hii itakayobakia muda mefu."
Hayo yamesemwa na msanii na mwanaharakati wa Qur'ani wa Iran Rain Khanzadeh aliyetengeneza Qur'ani ndogo zaidi iliyonakshiwa kwenye dhahabu. Qur'ani hiyo imeonyeshwa katika hoteli ya Burujul Arab huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Amesema, kazi ya kunakshi Qur'ani hiyo juu ya dhahabu imechukua muda wa miezi 12 na kuongeza kuwa ametumia kilo 5.8 za dhahabu ya daraja 22, vipande 8991 vya almasi, vipande 100 ya rubi na zumaridi kwa kadiri kwamba Qur'ani hiyo imekuwa athari na kazi ya kisanii isiyokuwa na kifani duniani.
Khanzadeh amesema utayarishaji wa kazi hiyo ya kisanii imegharibu tumani bilioni moja za Iran na kwamba ameitengeneza kutokana na hamu yake binafsi na kwa ajili ya kuhudimia sanaa ya Kiislamu na Kiirani.
Msanii huyo wa Iran amesema: "Baada ya Kasisi Terry Jones wa Marekani kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu na kutayarisha sherehe ya kuchoma moto kitabu hicho niliathiriwa mno na tukio hilo na nikachukua uamuzi wa kutayarisha kazi hii ya kisanii". 855714
captcha