Akizungumza hapo siku ya Alkhamisi, al- Qausi amesema kuwa ameafiki kufanyika kwa mashindano hayo ambayo huandaliwa kila mwaka na Taasisi ya Ab'rar Misr.
Mashindano hayo ambayo ni ya kitaifa hufanyika katika hatua tatu za kuhifadhi robo ya Qur'ani Tukufu, Qur'ani nzima na sura fupi za kitabu hicho kitakatifu. Ni walemavu wa akili tu ndio wanaoruhusiwa kushiriki katika mashindano hayo, na wanapasa kuwa wanachama wa mojawapo ya jumuiya na taasisi za kuwalinda walemavu wa akili nchini Misri.
Washiriki pia wanatakiwa kuwasilisha maombi yao ya maandishi kwa Tasisi ya Ab'rar Misr kabla ya kushiriki kwenye mashindano hayo ya kitaifa.
Walio na hamu ya kushiriki mashindano hayo wana hadi kufiki atarehe 22 Septemba kujiandikisha. Utangulizi wa mashindano hayo utafanyika kuanzia tarehe 18 Septemba hadi tarehe 13 Oktoba. Hatua ya mwisho ya mashindano hayo itafanyika tarehe 23 Oktoba hadi 27 Oktoba. 857259