IQNA

Mashindano ya 24 ya Qur'ani na Hadithi ya nchi za Ghuba ya Uajemi kufanyika

18:40 - September 14, 2011
Habari ID: 2187111
Mashindano ya 24 ya Qur'ani Tukufu na Hadithi ya nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi yamepangwa kufanyika tarehe 24 hadi 29 Septemba nchini Kuwait.
Kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo KUNA, mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Michezo na Vijana ya Kuwait PAYS, yatazijumuisha nchi za Ghuba ya Uajemi ambazo zitachuana katika mashindano tofauti ya Qur'ani na Hadithi. Faisal Jazaf, mkuu wa taasisi iliyotajwa amesema mipango ya kuandaa mashindano hayo ilianza muda mrefu uliopita na kwamba inatazamiwa kukamilika katika kipindi cha siku chache zijazo. Amesema taasisi hiyo tayari imekwishawachagua waamuzi ambao watasimamia mashindano hayo na pia kutoa mialiko kwa viongozi wa serikali na wa mashirika binafsi na yasiyokuwa ya kiserikali ili kuhudhuria shererhe za ufunguzi wa mashindano hayo muhimu. 860021
captcha