IQNA

Mahafidh wa Qur'ani nzima wa Kipalestina waenziwa

15:19 - September 19, 2011
Habari ID: 2189865
Zaidi ya mahafidhi wa Qur'ani Tukufu 50 wameenziwa na kushukuriwa katika tamasha maalumu lililoandaliwa na Kituo cha Mafunzo, Hifdhi ya Qur'ani na Hadithi za Mtume (saw) cha Ukanda wa Gaza.
Mahafidhi hao wapatao 53 walitunukiwa zawadi na kushukuriwa kutokana na juhudi zao za kuhifadhi Qur'ani nzima katika tamasha maalumu lililofanyika chini ya anwani ya 'Askari wa Qur'ani, Watetezi wa al-Aqsa.'
Viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas wakiwemo Zuhdi Abu Na'ma Wail az-Zard na Fauzi Burham walihudhuria tamasha hilo.
Sherehe za kuwaenzi mahafidhi hao zilipambwa kwa kasida za Kiislamu, usomaji Qur'ani Tukufu na hotuba za baadhi ya viongozi wa Hamas.
Akizungumza katika shehere hiyo, Wail az-Zard aliwasihi vijana na watu wa matabaka yote ya Palestina kutilia maanani mafundisho ya Qur'ani katika maisha yao ya kila siku. 863216
captcha