IQNA

Serikali ya Uturuki yaondoa sharti la umri katika kozi za Qur’ani

15:45 - September 21, 2011
Habari ID: 2191328
Serikali ya Uturuki imeondoa sharti la umri kwa watoto wanaotaka kuhudhuria kozi za Qur’ani zinazoendeshwa bila malipo katika misikiti nchini humo wakati wa msimu wa joto.
Kwa mujibu wa marekebisho ya sheria katika Idara ya Masuala ya Kidini sasa watoto walio chini ya umri wa miaka 12 wanarushusiwa kushirika katika masomo ya Qur’ani. Huko nyuma kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Februari 28 mwaka 1997, watawala wa kijeshi waliwakataza watoto waliokuwa na umri wa chini ya miaka 12 kushirika katika kozi za Qur’ani. Hatua hiyo ililaaniwa sana na wananchi Waislamu nchini Uturuki.
Sheria hiyo iliendelea kufanya kazi hata baada ya utawala huo wa kijeshi kuondolewa madarakani.
Hatua ya serikali ya Uturuki ya kuibatilisha sheria hiyo ni moja ya jitihada za serikali hiyo za kufuta kabisa sheria zilizopitishwa baada ya mapinduzi hayo ya kijeshi.
864517
captcha