Hayo ni kwa mujibu wa Danesh Sefatzadeh mkurugenzi wa magereza katika mkoa wa Hormozgan nchini Iran. Amesema matatizo mengi ya kijamii yanatokana na kutozingatiwa mafundisho ya kidini na Qur’ani.
Amesema kuwa idadi ya wafungwa itapungua iwapo thamani za kidini zitaenezwa katika jamii.
Sefatzadeh ameashiri nafasi ya Qur’ani Tukufu na utekelezwaji mafundishi yake katika maisha ya kila siku na kusema, hiyo ndio njia bora zaidi ya kupunguza matatizo ya kijamii.
Amesema kuwa kumekuwepo na vikao 4000 vya kuhitimisha Qur’ani katika magereza ya Hormozgan mbali na kuwepo mafunzo ya tajweed, qiraa, tafsiri, sheria za Kiislamu, akhlaqi na kuhifadhi hadithi.
864623