IQNA

Kongamano la ‘Avicenna na Wanafalsafa wa Kiislamu’

15:40 - September 21, 2011
Habari ID: 2191364
Kongamano lenye anwani ya ‘Avicenna na Wanafalsafa wa Kiislamu’ litafanyika Tehran Oktoba 18-19 chini ya usimamizi wa Taasisi ya Hekima ya Sadra ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa katibu wa kogamano hilo Qasim Pur Hassan, kongamano hilo litajadili nadharia za wanafalsafa wa Kiislamu waliokuja baada ya Farabi mwaka 550 Hijria.
Amesema kongamano hilo litakuwa na vitengo vitatu venye anwani ya ‘Kutoka Farabi hadi Avicenna, ‘Avicenna’ na ‘Kutoka Avicenna hadi Sohrawardi’.
Mkuu wa Taasisi ya Hekima ya Sadra ya Kiislamu Ayatullah Sayyod Mohammad Khamenei anatazamiwa kutoa hotuba katika ufunguzi wa mkutano huo.
864604
captcha