IQNA

13:54 - September 22, 2011
Habari ID: 2191874

Msanii wa Ufaransa aivunjia heshima Qur'ani, akiwa uchi wa mnyama

Msanii mmoja wa Ufaransa mwenye asili ya Morocco ameivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa kuandika kwenye mwili wake ulio uchi wa myama aya za kitabu hicho kitakatifu na kisha kuonyesha picha za kitendo hicho kichafu kupitia video projekta.

Kwa mujibu wa mtandao wa romande, msanii huyo Mahdi George Lahlu ambaye anajitayarisha kushiriki kwenye maonyesha ya kimataifa ya sanaa yaliyopewa jina la 'Sanaa ya Kisasa' huko Morocco amefanya kitendo hicho cha dharau dhidi ya moja ya matukufu ya Kiislamu na hivyo kuamsha hasira ya Waislamu duniani.
Baada ya kuonyeshwa picha hizo za dharau vijana wa Kiislamu wa Morocco wamewataka viongozi wa nchi hiyo na Ufaransa kuchukua hatua za dharura ili kumuadhibu msanii huyo.
Licha ya hayo, msanii huyo mwenye kiburu ametoa taarifa kupitia tovuti yake akitangaza kuwa atatuma picha hizo za dharau katika maonyesho yaliyotajwa yaliyopangwa kufanyika Morocco kati ya tarehe 30 Septemba hadi 3 Oktoba bila ya kuhudhuria yeye mwenyewe kwenye maonyesho hayo. 865113
captcha