Kituo cha habari cha Sunniforum kimeripoti kuwa vikao hivyo vya Qur'ani vilivyoanza tarehe 19 Septemba vitaendelea hadi tarehe 9 Oktoba.
Vikao hivyo vinafanyika katika misikiti ya New York, New Jersey na Pennsylvania na vinasimamiwa na Kituo cha Kiislamu cha Asifa chenye makao yake mjini New York.
Mkuu wa Madrasa ya Rahmaniya ya Dhaka, Bangladesh Hafidh Zubair Ansari na khatibu wa Msikiti wa Baitul Maamur wanatoa darasa za tafsiri ya Qur'ani katika vikao hivyo. 867421