Duru ya kwanza ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu kwa wanafunzi wa shule za msingi nchini Iraq ilianza siku ya Jumapili katika mji mtakatifu wa Kadhimain ambapo shakhsia mashuhuri wanaoshughulikia masuala ya Qur'ani Tukufu, ya kidini na kiutamaduni walihudhuria.
Mashindano hayo yamepangwa kuendelea kwa muda wa siku nne. Ra'd Adnan an-Nassiri, mratibu wa Kamati Kuu ya Qur'ani Tukufu iliyoko chini ya sekeitarieti ya Baraza la Mawaziri la Iraq katika mkoa wa Dhi Qar amesema kwamba mashindano hayo yanayowashirikisha wanafunzi kutoka mikoa yote ya nchi hiyo yanadhaminiwa na ofisi ya Ayatullahil Udhma Shahid Sayyid Muhammad Baqir Sadr.
Mashindano ya utangulizi ya mashindano yanayofanyika sasa yalifanyika huko nyuma katika mikoa yote ya Iraq na washindi wa mashindano hayo kuandaliwa fursa ya kushiriki kwenye mashindano yanayoendelea sasa katika mji uliotajwa.
Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi wa mashindano hayo, Muhammad Musa, Mkurugenzi Mkuu wa Vituo vya Malezi ya Walimu vinavyofungamana na Wizara ya Elimu na Malezi ya Iraq amesema kuwa kufanyika kwa mashindano kama hayo ya Qur'ani Tukufu kuna nafasi muhimu katika kuimarisha uhusiano wa taasisi za masomo na kidini za nchi hiyo. 867697