IQNA

Nakala zenye makosa za Qur'ani zakusanywa Saudia

19:44 - September 28, 2011
Habari ID: 2195244
Mkurugenzi wa kiwanda cha uchapishaji wa Qur'ani cha Mfalme Fahad nchini Saudi Arabia amesema kuwa nakana za Qur'ani ya elektroniki zenye makosa ya kichapa zimeanza kukusanywa.
Muhammad bin Salim Shadidi al Aufi amesema kuwa kiwanda hicho kimetoa amri ya kukusanywa na kurejeshwa nakala zote za Qur'ani ya elektroniki zenye makosa ya kichapa.
Al Aufi amesema kuwa Wizara ya Utamaduni na Habari ya Saudi Arabia ndiyo inayowajibika kuzuia uingizaji wa nakala hizo za Qur'ani zenye makosa ya kichapa. 869272

captcha