Akihutubu katika khitma hiyo iliyohudhuriwa na Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri Mkuu wa Jumuiya ya Kuyakurubisha Madhehebu ya Kiislamu pamoja na idadi kubwa ya Mujahidina wa Afghanistan, Balozi wa Afghanistan mjini Tehran ameashiria shakhsia ya Shahidi Rabbani na kusema daima alipinga upotofu.
Amesema Shahidi Rabbani alisisitiza sana umuhimu wa Umoja wa Kiislamu duniani katika hotuba yake ya mwisho alipokuwa akihutubia mkutano wa Mwamko wa Kiislamu mjini Tehran.
Rabbani aliuawa shahidi katika hujuma ya bomu nyumbani kwake Septemba 20 mjini Kabul siku mbili tu baada ya kuhudhuria kikao cha mwamko wa Kiislamu mjini Tehran.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa ya Afghanistan wanakuelezea kuuawa shahidi Burhanuddin Rabbani kuwa ni uendelezaji wa silsili ya mauaji ya kigaidi ya shakhsia wa Jihadi nchini Afghanistan na wapinzani wa mkataba wa usalama uliofikiwa kati ya nchi hiyo na Marekani ambao Washington inatumia kila njia kuitwisha serikali ya Kabul iutekeleze.
Tokea takribani miaka mitatu nyuma, imeanza harakati ya kuwaua shakhsia wa Jihadi ambao walifanya jitihada kubwa kwa ajili ya uhuru na ukombozi wa Afghanistan; na kwa kuzingatia njama na uadui wa Marekani dhidi ya wananchi wa Afghanistan, mauaji ya kigaidi ya Rabbani hayatazamiwi kuwa utakuwa ndio mwisho wa kuwaangamiza mujahidina wa Afghanistan. Suala hili limeshazungumziwa mara kadha wa kadha na viongozi wa serikali ya Kabul pamoja na shakhsia mbalimbali wa jihadi wa nchi hiyo. Wakati akihutubia katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi shujaa wa taifa Ahmad Shah Masoud, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Afghanistan Muhammad Qasim Fahim alitahadharisha juu ya njama za adui za kuwamaliza wanajihadi, na kuitaka serikali ichukue hatua za kukabiliana na harakati hiyo chafu na ovu. Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimeanzisha kampeni kubwa za kuwaua shakhsia wa Jihadi nchini Afghanistan ili kwa kufanya hivyo kufuta dhana ya muqawama katika nchi hiyo. Lakini hakuna shaka yoyote kuwa kuuawa shahidi mujahidina halisi wa uhuru na ukombozi wa Afghanistan kutazidi kuwafanya wananchi na hasa vijana wawe na ari na moyo zaidi wa kuendeleza njia yao. Mahudhurio makubwa ya wananchi wa Afghanistan katika maziko ya Burhanuddin Rabbani yanaweza kutathminiwa katika muelekeo huo
868500