IQNA

Wabahrain wasusia uchaguzi wa Bunge

10:43 - October 02, 2011
Habari ID: 2197071
Wananchi wa Bahrain wamesusia duru ya pili na ya mwisho ya uchaguzi mdogo wa Bunge uliokumbwa na matatizo makubwa katika nchi hiyo ya kifalme ya Ghuba ya Uajemi.
Mashirika ya habari yamewanukuu watu walioshuhudia wakisema kuwa, watu wasiofika hata 12 wamejitokeza katika uchaguzi uliodumu kwa dakika 20 tu katika kituo kikuu cha kupigia kura kwenye kijiji cha Sehla.
Wakati huo huo mtu mmoja tu ndiye aliyejitokeza kupiga kura katika muda kama huo kwenye kijiji cha Sanabes.
Serikali ya familia ya kifalme ya Aal Khalifa nchini Bahrain imeitisha uchaguzi mdogo ili kujaza nafasi za Wabunge 18 kutoka chama kikubwa cha upinzani cha al Wifaq ambao walijitoa Bungeni kulalamikia ukandamizaji wa utawala wa familia ya kifalme ya Aal Khalifa nchini Bahrain unaosaidiwa na familia ya kifalme ya Aal Saud.
Hata ukurasa wa Intaneti wa serikali ya Bahrain unaohusiana na uchaguzi umekiri kuwa watu waliojitokeza kwenye uchaguzi huo mdogo ni wachache mno.
Bahrain imekuwa ikikabiliwa na maandamano makubwa ya wananchi ambao wamechoshwa na kutawaliwa na familia moja tu, wakitaka kubadilishwa mfumo wa utawala nchini humo. 871335
captcha