IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iraq yakamilisha kazi zake

10:52 - October 03, 2011
Habari ID: 2197875
Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iraq ambao yamepewa jina na "Kunusuru Qur'ani Tukufu" yalimalizika jana katika mji wa Kadhimein.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Darul Qur'ani ya mji wa Nasiriyya nchini Iraq Raad Adnan amesema kuwa msomaji wa Iraq Sayyid Mahdi ameshinda nafasi ya kwanza katika hifdhi ya Qur'ani akifuatwa na msomaji wa Iran Ali Ridha Zadeh ambaye ameshika nafasi ya pili. Nafasi ya tatu katika hifdhi ya Qur'ani imechukuliwa na karii kutoka Misri Husam Marzouk.
Katika upande wa kiraa, msomaji Usama Abdul Hamza kutoka Iraq ameshinda nafasi ya kwanza ya mashindano hayo ya kimataifa akifuatiwa na Hussain Yazdanpanah kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Khalid Muhamad Hanafi kutoka Misri ameshika nafasi ya tatu.
Jopo la majaji wa mashindano hayo lilijumuisha karii mashuhudiri wa Misri Abdul Fattah Taruti.
Mashindano hayo ya kwanza ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iraq yalisimamiwa na Ofisi ya Ayatullahil Udhmaa Shahid Muhammad Baqir al Sadr na kuwashirikisha makarii na mahafidhi kutoka nchi 16. 871785

captcha