IQNA

Nuskha za Qur'ani zilizo na makosa zaonyeshwa katika maonyesho ya Algeria

16:38 - October 04, 2011
Habari ID: 2198881
Nuskha za Qur'ani Tukufu zilizo na kasoro za kurasa na aya, zilizopitishwa na Jumuiya ya Utafiti ya al-Azhar zimeonyeshwa katika maonyesho ya 16 ya kimataifa ya vitabu nchini Algeria.
Katika nuskha hizo zaidi ya kurasa 30 na aya 200 za Suratul Baqara zimedondoka kwa maana kwamba kurasa za nne hadi 35 za Qur'ani yaani tokea aya ya 16 hadi 226 za suratul Baqara zimedondoka.
Wageni wanaotembelea maonyesho hayo wamelalamikia vikali suala hilo na kuikosoa kamati inayosimamia maonyesho hayo kwa kuruhusu nuskha hizo za Qur'ani kuonyeshwa kwenye maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yaliyoanza tarehe 21 Septemba yakiyajumuisha mashirika ya uchapishaji 512 yakiwemo 376 ya kigeni kutoka nchi 35 za dunia yalimalizika tarehe Mosi Oktoba. 872685
captcha