IQNA

Mashindano ya taifa ya Qur'ani kufanyika Algeria

14:30 - October 05, 2011
Habari ID: 2199570
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Algeria imetangaza kuwa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya maimamu na walimu wa Qur'ani yatafanyika hivi karibuni nchini humo.
Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya Algeria imesema kuwa mashindano hayo yatafanyika tarehe 12 hadi 18 Oktoba katika miji kadhaa ya nchi hiyo. Mashindano hayo yatafanyika katika sehemu mbili tofauti kwa ajili ya maimamu na viongozi wa misikiti na walimu wa Qur'an Tukufu.
Maimamu 300 wa misikiti, walimu 140 wa Qur'ani, waadhini na maafisa wa taasisi na jumuiya za Kiislamu 235 watashiriki katika mashindnao hayo. 873991

captcha