Kwa sasa kituo hicho cha kuchapisha Qur'ani kinachunguza mipango ya kuitisha kongamano hilo ambalo litafanyika katika siku chache zijazo.
Watu, taasisi, vyombo rasmi na visivyokuwa rasmi vinavyojishughulisha na masuala ya Qur'ani kutoka nchi mbalimbali vitaalikwa kushiriki katika kongamano hilo. Kongamano hilo litajadili na kuchunguza tafiti na tajiriba za washiriki katika medani ya uchapishaji wa Qur'ani Tukufu.
Katibu Mkuu wa Kituo cha Kuchapisha Qur'ani cha Mfalme Fahad Muhammad Salim bin Shadid al Aufi amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kukutanisha pamoja wanaharakati wa masuala ya uchapishaji Qur'ani kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kupasisha sheria, kanuni na mbinu bora zinazokubalika na pande zote kwa ajili ya kuchapisha Qur'ani Tukufu, sheria ambazo zitatekelezwa kote duniani.
Amesema kuwa kongamano hilo ni katika juhudi za kuzuia uchapishaji wa nakana za Qur'ani zenye makosa ya kimaandishi.
875607