Kituo cha habari cha Lexpressiondz kimeripoti kuwa kundi hilo la Wazayuni lilishambulia makaburi hayo ya Waislamu na Wakristo mapema jana na kuharibu makaburi kadhaa na kuandika maneno machafu dhidi ya Waislamu na Wakristo juu ya makaburi mengine.
Makaburi 22 ya Waislamu na 4 ya Wakristo yalivunjwa na kuhabribiwa katika shambulizi hilo na matukufu ya dni hizo mbili yamevunjiwa heshima.
Wakazi wa mji wa Yafa katika ardhi zilizovamiwa na Wazayuni wa Israel mwaka 1948 wamelaani shambulizi hilo na kusema kuwa hatua hiyo itachochea hisia za Waislamu na kuzusha machafuko.
Katika wiki za hivi karibuni misikiti kadhaa ya Waislamu wa Palestina imechomwa moto na walowezi wa Kiyahudi na inaonekana kuwa kuvunjiwa heshima makaburi ya Waislamu na Wakristo ni mwanzo wa wimbi jipya la ukatili na ubaguzi wa Wazayuni wa Israel. 876059