IQNA

Nakala za Qur'ani za hati ya Braille zasambazwa Palestina

15:47 - October 10, 2011
Habari ID: 2202479
Idara ya Mwongozo na Malezi ya Wizara ya Elimu ya serikali halali ya Palestina imegawa nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za Braille makhsusi kwa ajili ya vipofu.
Nakala hizo zimetolewa kwa wanafunzi 38 wa kike na kiume wa shule ya vipofu ya al Nour wal Amal.
Sherehe za kugawa nakala hizo za Qur'ani makhsusi kwa watu vipofu zimehuduriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Wizara ya Elimu ya Palestina.
Naibu Waziri wa Elimu wa Palestina Ziad Thabit amesema kugawa Qur'ani hizo kwa wanafunzi vipofu kunawapa fursa ya kusoma Qur'ani Tukufu, kuhifadhi kitabu hicho na hata kushiriki katika mashindano ya Qur'ani.
Amesema kuwa uzoefu umethibitisha kuwa wanafunzi wenye ulemavu wa macho wanafanya vizuri zaidi katika mashindano ya sayansi ya Qur'ani kuliko wenzao wasiokuwa na ulemavu huo. 876987


captcha