IQNA

Viongozi wa Sudan na Qatar kuchunguza matukio ya kieneo

16:19 - October 10, 2011
Habari ID: 2202508
Rais Omar al-Bashir wa Sudan amewasili nchini Qatar kwa lengo la kujadiliana na viongozi wa nchi hiyo kuhusiana na matukio ya kieneo na pia kuimarisha uhusiano wa pande mbili.
Serikali ya Sudan imetangaza kuwa safari hiyo ambayo pia itawajumuisha viongozi wengine wa ngazi za juu wa serikali ya Khartoum itaendelea kwa muda wa siku mbili.
Mazungumzo hayo ya siku mbili yanafanyika huku Qatar ikiwa mpatanishi kati ya serikali ya Khartoum na waasi wa eneo la Darfur la magharibi mwa nchi hiyo.
Miezi kadhaa iliyopita Qatar ilikuwa mwenyeji wa pande hizo hasimu za Sudan ambapo serikali ya Khartoum hatimaye ilifikia mapatano ya suluhu na Harakati ya Uhuru na Uadilifu ya Darfur. 876885
captcha