Afisa anayehusika kutoa vibali vya kuchapisha Qur'ani katika Kituo cha Kiislamu cha al Azhar Dhiauddin Muhammad amesema kuwa amri ya kukusanywa nakala zote za Qur'ani zilizochapishwa China imetolewa kutokana na makosa ya kichapa na kimaandishi yaliyomo katika nakala hizo.
Ameongeza kuwa nakala hizo za Qur'ani kutoka China zinazouzwa kwa bei ya chini katika masoko ya Misri zimejaa makosa makubwa ambayo hayawezi kufumbiwa macho.
Afisa huyo wa al Azhar amezitaka nchi za Kiislamu kuchukua msimamo mmoja wa kuilazimisha China isitishe uchapishaji wa nakala za Qur'ani na kuongeza kuwa hatua kali zinapaswa kuchukuliwa ili tusije kuona Israel pia inachapisha nakala za Qur'ani na kuzigawa bure. 878055