IQNA

14:41 - October 12, 2011
Habari ID: 2203757

Mkuu wa televisheni ya Nasma ya Tunisia awaomba radhi Waislamu

Nabil Karwawi, Mkurugenzi Mkuu wa Televisheni ya Nasma ya nchini Tunisia amewaomba radhi Waislamu wa nchi hiyo kwa kurusha hewani filamu iliyo dhidi ya Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inayoitwa Persepolis.

Akizungumza mbele ya waandishi habari hapo jana Jumanne, Karwawi amesema kuwa hatua ya kuonyeshwa filamu hiyo inayomwonyesha Mwenyezi Mungu akiwa katika kalibu ya sura ya mwanadamu, ni makosa makubwa ambayo yalifanywa na wasimamizi wa televisheni hiyo.
Nabil Karwawi amesema kuwa halikuwa kusudio la televisheni hiyo kuvunjia heshima matukufu na thamani za kidini za Watunisia.
Mkuu wa Televisheni ya Nasma pia ametoa taarifa maalumu akiwataka wananchi wa nchi hiyo kuwa watulivu na kutoruhusu filamu hiyo kuzusha ghasia nchini. Amewataka kufuatilia suala hilo kupitia vyombo husika vya kisheria.
Wakati huohuo, Mwendesha Mashtaka wa Tunisia amesema kuwa tayari idara yake imewasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya televisheni hiyo kwa kukiuka misingi ya Uislamu.
Kufuatia kuonyeshwa filamu hiyo inayoudhihaki Uislamu, umati mkubwa wa Watunisia umekusanyika mbele ya jingo la Televisheni ya Nasma na kulalamikia vikali kitendo cha televisheni hiyo cha kukanyaga misingi ya dini tukufu ya Kiislamu. 878362
captcha