IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo Waislamu kufanyika Lebanon

15:23 - October 12, 2011
Habari ID: 2203857
Mkuu wa Jumuiya ya Shughuli za Kiqur'ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Iran ametoa pendekezo la kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu nchini Lebanon. Mashindano hayo ya 4 ya wanachuo Waislamu yamepangwa kufanyika mwezi Mei mwakani.
Kadhia hiyo ilijadiliwa katika mazungumzo ya Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mahdi Taqawi Mkuu wa Jumuiya ya Shughuli za Kiqur'ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Iran na Hujjatul Islam Ali Arif ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya Lebanon.
Sayyid Taqawi amesema katika mazungumzo hayo kwamba shirika la habari la IQNA ndilo shirika pekee linaloshughulikia kitaalamu habari za Qur'ani kote duniani na kwa sasa lina vitengo vya lugha 35 hai za dunia vinavyofikisha ujumbe wa Qur'ani Tukufu kwa walimwengu.
Amesema Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani la IQNA linafuatiliwa kwa wingi katika maeneo mbalimbali duniani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya Lebanon amekaribisha fikra ya kufanyika mashindano ya 4 ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo Waislamu nchini humo. 878367
captcha