Akizungumza katika sherehe hizo, Muhammad Matwar Tarim, mkuu wa Taasisi ya Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw) ya Sharjah amesema mashindano ya mwaka huu yaliwajumuisha wahifadhi wengi zaidi wa Qur'ani na Hadithi ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Ameongeza kwamba hatimaye ni washindi wa mwisho 45 ndio waliofanikiwa kuingia katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo kati ya washindi wengi walioshiriki katika makundi tofauti ya kuhifadhi Qur'ani na Hadithi, kiraa, tajwidi, tafsiri na maana ya maneno ya Qur'ani na Hadithi.
Amesema kushiriki kwa wasomaji na mahafidhi mashuhuri wa Qur'ani katika mashindano hayo ya kila mwaka ni ishara ya wazi kwamba waandaaji wa mashindano hayo wamefanikiwa katika malengo yao ya kulea kizazi bora kilichohifadhi na kufahamu maana ya aya za Qur'ani na Hadithi za Mtume (saw). 878682