IQNA

Saudia kuchukua alama za vidole za mahujaji wote

16:34 - October 16, 2011
Habari ID: 2205981
Mahujaji wote wanaoelekea Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada muhimu ya Hija watachukuliwa alama za vidole na utawala wa nchi hiyo.
Watawala wa Saudi Arabia wanadai kuwa wanatekeleza hatua hiyo ya kiusalama kwa lengo la kuzuia kuingia katika miji mitakatifu ya Makka na Madina watu wasio na vibali rasmi.
Akifafanua suala hilo Ayedh bin Taghalib, mkuu wa idara ya kutoa viza za hija amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, uchukuaji wa alama hizo za vidole utafanyika katika vituo vyote vya kuingia na kutoka Saudi Arabia. Amesema maafisa waliopewa mafunzo maalumu wametumwa kwenye vituo hivyo ili kuzuia kuingia nchini humo watu wasio na vibali halali.
Inavyoonekana ni kuwa watawala wa nchi hiyo wamechukua hatua hiyo ya kiusalama kutokana na wasiwasi wao kuhusiana na athari za mapinduzi yanayoendelea katika nchi kadhaa za Kiarabu na vilevile ghasia zilizozuka hivi karibuni katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo. 880597
captcha