IQNA

Nchi 52 kushiriki katika mashindano ya 32 ya kimataifa ya Qur'ani Saudia

17:07 - October 17, 2011
Habari ID: 2206676
Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Wakfu na Mwongozo ya Saudi Arabia imetangaza kuwa wawakilishi wa nchi 52 dunia watashiriki katika mashindano ya 32 ya kimataifa ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani yatakayofanyika nchini humo.
Wizara hiyo imetoa taarifa ikitangaza majina na nchi zitakazoshiriki katika mashindano hayo.
Katibu wa mashindano hayo Mansour bin Muhammad al Samii amesema kuwa makarii 154 kutoka nchi 52 watachuana katika nyanja mbalimbali za mashindano hayo.
Ameongeza kuwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Saudi Arabia yanafanyika kwa lengo la kuwahamasisha vijana kushikamana na Qur'ani, kuhifadhi, kutaamali aya za kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kuimarisha moyo wa ushindani kati ya mahafidhi wa Qur'ani Tukufu.
Mashindano ya 32 ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani ya Saudia yatafanyika katika mwezi wa Muharram mwaka 1433 Hijria katika mji mtakatifu wa Makka. 881409

captcha